Furaha ya Ajabu
Furaha ya Ajabu |
---|
Performed by | - |
Category | Harusi |
Views | 4,059 |
Furaha ya Ajabu Lyrics
- Furaha ya ajabu, pia na vigelegele,
kwa hao ndugu zetu, wanaoona.
Wanathibitisha kuwa wataishi kama mke na mme *2
Mmethibitisha mbele ya kanisa
ya kwamba mtaishi na mkipendana
Siku zote daima na milele
Tunawatakia amani ya Bwana
na upendo wake ukae na nyinyi
Siku zote daima na milele
(Tenor) Mmeahidi
All Mmeahidi kwamba mtaishi
(Tenor) Katika mema
Katika mema na katika mabaya
(Tenor) Mmeahidi
All Mmeahidi kwamba mtaishi
(Tenor) Kwa utajiri
Kwa utajiri na umaskini
(Tenor) Mmeahidi
All Mmeahidi kwamba mtaishi
(Tenor) Mpaka kifo
Mpaka kifo kitakapowatenga
- Mmepewa pete ya kuwa ni ukumbusho alama ya ahadi ya ndoa yenu
Ya kwamba mtaishi na mkipendana mpaka kifo chenu *2
Mmethibitisha mbele ya kanisa ya kwamba mtaishi na mkipendana
Siku zote daima na milele
Tunawatakia amani ya Bwana na upendo wake ukae na nyinyi
Siku zote daima na milele