Mema Yote

Mema Yote
Performed by-
CategoryHarusi
Views3,492

Mema Yote Lyrics

 1. Mema yote Baba uwajalie -
  Baba walinde vyema maisha yao yote *2
  Ndoa yao Mungu uibariki -
  Moyoni mwao pendo liwe siku zote

  Harusi - harusi ni siri kati yenu
  Upendo - awajalie Mungu mwenyezi. *2

 2. Nawe Bwana uwe mwaminifu -
  Kwake mkeo Yesu akikuongoza. *2
  Umtunze vyema maisha yote -
  Haki na kweli ziwe ndizo msingi wenu *2
 3. Mwanamke mzuri ni tabia -
  Baba motto wako ameapa kwako *2
  Atakuwa mke mwenye busara -
  Nyumbani mwake pendo litajaa tele. *2