Ndiwe Sitara Yangu
Ndiwe Sitara Yangu Lyrics
{Ndiwe sitara yangu Bwana
Utanihifadhi na mateso
Utanizungusha nyimbo za wokovu
Nyimbo za wokovu } *2
- Nalia mchana kutwa, nalia usiku kucha
Lakini nafuu sipati Bwana usinitupe
- Bwana ni mdudu, wala si mtu kabisa
Nimepuuzwa na kudharauliwa na kila mtu
- Ulimi wangu wang'ata kinywani mwangu ee Bwana
Umeniacha kama mpumbavu mimi ninaangamia
- Bwana wewe ulitoa, Bwana wewe umetwaa
Nichukue nami nikapumzike pema peponi
- Atukuzwe Mungu Baba, na mwanaye mtukuka
Atukuzwe na Roho Mtakatifu milele amina