Nchi Inazizima
| Nchi Inazizima | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | Bernard Mukasa |
| Views | 14,258 |
Nchi Inazizima Lyrics
Yuda akarudi, chukua fedha zenu huyu ni mwema,
Pilato akakiri hana kosa lakini kamuueni,
Kainuliwa mtupu na kajeruhiwa sana,
Amekata roho, nchi inazizima kwa huzuni kuu.- Ona damu, mwili umelowana
Ona nyama, madonda mwili mzima
Moyo wake, nao umetoboka.
Mate yao, yamemfunika uso. - Meno yake, kang'ata kwa uchungu.
Nafsi yangu, imemjeruhi Yesu
Dhambi zangu, zikamchomoa roho
Mungu wangu, nionjeshe uchungu - Ili nife, pamoja naye Kristu
Mwisho nije, nikafufuke naye