Mungu Wangu Mbona Umeniacha

Mungu Wangu Mbona Umeniacha
Performed bySt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerG. A Chavalla
Views37,231

Mungu Wangu Mbona Umeniacha Lyrics

  1. Mungu wangu mbona umeniacha mimi
    Katika taabu zote hizi
    Maisha yangu ni ya mashaka
    Kwani sina raha nimekosa amani
    Matatizo mengi yananisonga (sana)
    Nakuomba Bwana nisaidie
    Maadui zangu wananiwinda (kutwa)
    Wanitega ili wanikamate

    Ninalala macho wazi mimi (kama ndege)
    Kama ndege mkiwa juu ya paa
    Nimekuwa kama mhuni mimi (fanya hima)
    Fanya hima Bwana kuniokoa

  2. Nimekuwa kama kichekesho kwa watu jamani mimi Bwana
    Kila nipitapo hunisema na kunicheka
    Wananizushia maneno ya uongo jamani mimi Bwana
    Mimi nimekuwa ni jalala la kila baya
  3. Maadui zangu kutwa wanisimanga jamani mimi Bwana
    Wananidhihaki wanisonya na kunitusi
    Jina langu limekuwa gumzo lao jamani mimi Bwana
    Sasa ndilo walitumialo kwa kulaania
  4. Na majivu yamekuwa chakula changu jamani mimi Bwana
    Na machozi yangu yamekuwa kinywaji changu
    Na siku zangu zinapita kama moshi jamani mimi Bwana
    Nakuomba usinichukue bado kijana