Mungu Wangu Mbona Umeniacha

Mungu Wangu Mbona Umeniacha
ChoirSt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerG. A Chavalla
SourceTanzania

Mungu Wangu Mbona Umeniacha Lyrics

Mungu wangu mbona umeniacha mimi
Katika taabu zote hizi
Maisha yangu ni ya mashaka
Kwani sina raha nimekosa amani
Matatizo mengi yananisonga (sana)
Nakuomba Bwana nisaidie
Maadui zangu wananiwinda (kutwa)
Wanitega ili wanikamate

Ninalala macho wazi mimi (kama ndege)
Kama ndege mkiwa juu ya paa
Nimekuwa kama mhuni mimi (fanya hima)
Fanya hima Bwana kuniokoa

 1. Nimekuwa kama kichekesho kwa watu jamani mimi Bwana
  Kila nipitapo hunisema na kunicheka
  Wananizushia maneno ya uongo jamani mimi Bwana
  Mimi nimekuwa ni jalala la kila baya
 2. Maadui zangu kutwa wanisimanga jamani mimi Bwana
  Wananidhihaki wanisonya na kunitusi
  Jina langu limekuwa gumzo lao jamani mimi Bwana
  Sasa ndilo walitumialo kwa kulaania
 3. Na majivu yamekuwa chakula changu jamani mimi Bwana
  Na machozi yangu yamekuwa kinywaji changu
  Na siku zangu zinapita kama moshi jamani mimi Bwana
  Nakuomba usinichukue bado kijana