Ee Mungu Baba Upokee Sadaka
Ee Mungu Baba Upokee Sadaka |
---|
Performed by | - |
Album | Viuzeni Mlivyo Navyo |
Category | TBA |
Composer | Joseph Makoye |
Views | 8,374 |
Ee Mungu Baba Upokee Sadaka Lyrics
{Ee Mungu Baba upokee sadaka
Sadaka safi isiyo na doa
Ni sadaka yake Mwanao mpenzi
Uliyependezwa naye } *2
- Ni ajabu ya sadaka hii
Mkate kugeuka mwili wake Yesu
Na divai kugeuka damu yake
- Ni sadaka ya agano jipya
Sadaka ya Bwana wetu Yesu Kristu
Iliyotolewa ili tuokoke
- Mungu Baba tunakutolea
Sadaka yetu hii kama ukumbusho
Wa sadaka aliyoitoa Yesu