Nirudieni Mimi

Nirudieni Mimi
Alt TitleLakini Hata Sasa
Performed byMalaika Mkuu Mikaeli Chang'ombe
AlbumMwanga wa Mataifa
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerAloyce Goden
Views60,235

Nirudieni Mimi Lyrics

  1. {Lakini hata sasa, asema Bwana
    Nirudieni mimi, kwa mioyo yenu yote } *2

  2. Fanyeni mabadiliko mioyoni mwenu
    Kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza
    Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote
  3. Pigeni tarumbeta huko Sayuni
    Wambieni watu wote ili wafunge
    Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote
  4. Kusanyeni watu wote waleteni kwangu
    Waleteni na watoto hata na wazee
    Nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote
  5. Mpingeni yule mwovu atawakimbia
    Nikaribieni nami nitawakaribia
    Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote
  6. Takaseni mikono yenu iliyojaa dhambi
    Safisheni mioyo yenu yenye nia mbili
    Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote