Bwana Aliridhika Kumchubua
| Bwana Aliridhika Kumchubua | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | Charles Saasita |
| Views | 2,958 |
Bwana Aliridhika Kumchubua Lyrics
Bwana aliridhika kumchubua, amemhuzunisha
Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu, dhabihu kwa dhambi
{Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi
Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake } *2- Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake
Na kuridhika, na kuridhika
Naye atayachukua maovu yao - Kwa maarifa yake mtumishi wangu
Ataridhika, ataridhika
Naye atafanya wengi kuwa wenye haki