Matumaini ya Safari
| Matumaini ya Safari | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Album | Matumaini ya Safari | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Composer | Marcus Mtinga | 
| Views | 10,634 | 
Matumaini ya Safari Lyrics
- Matumaini ya safari yetu, sasa yameingia dosari
 Kwani meli tuliyopanda, kuja kwako,
 Tazama imevamiwa na majambazi
 Hatuna njia nyingine itakayotuokoa kwenye janga hili
 Yesu mwema njoo haraka, utuokoe wanao tunakwisha wote
- Gonjwa hatari, lisilotibika, ona linatumaliza wote
 Halichagui halibagui, linafyeka,
 Ukimwi, halina huruma kwa wanadamu
 Limeua watu wengi, ni wengi wakubwa kwa wadogo wamepotea
 Milenia tuliyomaliza, ilijaa huzuni na majonzi kila upande
- Wanasayansi madaktari, wanaahangaika kutwa kucha
 Juhudi zinagonga mwamba, hakuna dawa
 Ee Bwana tunakufa tuonee huruma
 Tunaomba Mungu Mwenyezi, ingilia katika uwezo wako wote
 Macho yao uyafumbue, fanaka ipatikane, Bwana tunakuomba
- Tumeshaomba, tumesali sana, ee Bwana sikia sala zetu
 Tunaungama tumekosa Mungu Mwenyezi,
 tazama, Tunakulilia tusikilize
 Tunakufa kama nzige, ee Mungu ee Bwana tunateketea wote
 Si Sodoma wala Gomora, jamani hili linazidi tena latisha
- Ee Yesu Mwema, mwenye huruma, tunakuomba ututazame
 Damu na maji vilivyotoka mwilini mwako
 Zilete dawa halisi ya kutuponya
 Watoto ni wengi sana wanakufa bila ya hatia, inasikitisha
 Wengine sasa ni yatima, hawajui wataishi vipi maisha yao
- Tunakuomba, ee Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu
 Milenia tuliyoianza, njoo Bwana,
 Haraka ukatawale mioyo yetu
 Machozi tunayolia yafute maovu yetu yote kwa neema yako
 Lakini mapenzi yako yatimizwe vile utakavyotuashiria
 
  
         
                            