Matumaini ya Safari

Matumaini ya Safari
ChoirTBA
AlbumMatumaini ya Safari
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerMarcus Mtinga

Matumaini ya Safari Lyrics

 1. Matumaini ya safari yetu, sasa yameingia dosari
  Kwani meli tuliyopanda, kuja kwako,
  Tazama imevamiwa na majambazi
  Hatuna njia nyingine itakayotuokoa kwenye janga hili
  Yesu mwema njoo haraka, utuokoe wanao tunakwisha wote
 2. Gonjwa hatari, lisilotibika, ona linatumaliza wote
  Halichagui halibagui, linafyeka,
  Ukimwi, halina huruma kwa wanadamu
  Limeua watu wengi, ni wengi wakubwa kwa wadogo wamepotea
  Milenia tuliyomaliza, ilijaa huzuni na majonzi kila upande
 3. Wanasayansi madaktari, wanaahangaika kutwa kucha
  Juhudi zinagonga mwamba, hakuna dawa
  Ee Bwana tunakufa tuonee huruma
  Tunaomba Mungu Mwenyezi, ingilia katika uwezo wako wote
  Macho yao uyafumbue, fanaka ipatikane, Bwana tunakuomba
 4. Tumeshaomba, tumesali sana, ee Bwana sikia sala zetu
  Tunaungama tumekosa Mungu Mwenyezi,
  tazama, Tunakulilia tusikilize
  Tunakufa kama nzige, ee Mungu ee Bwana tunateketea wote
  Si Sodoma wala Gomora, jamani hili linazidi tena latisha
 5. Ee Yesu Mwema, mwenye huruma, tunakuomba ututazame
  Damu na maji vilivyotoka mwilini mwako
  Zilete dawa halisi ya kutuponya
  Watoto ni wengi sana wanakufa bila ya hatia, inasikitisha
  Wengine sasa ni yatima, hawajui wataishi vipi maisha yao
 6. Tunakuomba, ee Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu
  Milenia tuliyoianza, njoo Bwana,
  Haraka ukatawale mioyo yetu
  Machozi tunayolia yafute maovu yetu yote kwa neema yako
  Lakini mapenzi yako yatimizwe vile utakavyotuashiria