Kilio cha Damu
| Kilio cha Damu | |
|---|---|
| Alt Title | Mate Yakamkauka | 
| Performed by | - | 
| Album | Yowe la Mwisho | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 3,760 | 
Kilio cha Damu Lyrics
- Mate yakamkauka, moyo ukaganda,
 Na akakumbuka hali ya bustani Getsemani
 Mwili wake ulipotona jasho la damu
 Ngozi ikasinya, roho ikalia
 Na akang'ata meno kwa maumivu makali
 Kovu za misumari zilipouma upya
 Maisha ya vijana wa leo, yanatonesha majeraha ya Yesu
 Yale matendo yamo kwa giza, yanamliza kilio cha damu
- Akatazama kwenye kwenye vijiwe
 Vijana wamevuta wamelewa
 Kaona nyumba za wageni
 Wenyeji wanagawana ukimwi
- Kwa zahanati kuna foleni
 Vijana wanavinyonga vichanga
 Usiku kucha, dodo mapanga
 Vijana watafuta utajiri
- Wengine hao barabarani
 Wanauza hekalu la Roho Mungu
 Kisigizio, ajira haba
 Wateja wao ni wazazi wao
- Na majasira wanageuza
 Miili yao kufanya mabomu
 Wakidanganywa ati dhawabu
 Kumbe adhabu wanajitwalia
- Tubuni sana salini ninyi
 Jahazi lenu limeshatoboka
 Ombeni yeye awahifadhi
 Kwenye tundu la ubavuni mwake
 
  
         
                            