Kilio cha Damu

Kilio cha Damu
Alt TitleMate Yakamkauka
ChoirTBA
AlbumYowe la Mwisho
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
SourceTanzania

Kilio cha Damu Lyrics

Mate yakamkauka, moyo ukaganda,
Na akakumbuka hali ya bustani Getsemani
Mwili wake ulipotona jasho la damu
Ngozi ikasinya, roho ikalia
Na akang'ata meno kwa maumivu makali
Kovu za misumari zilipouma upya
Maisha ya vijana wa leo, yanatonesha majeraha ya Yesu
Yale matendo yamo kwa giza, yanamliza kilio cha damu

 1. Akatazama kwenye kwenye vijiwe
  Vijana wamevuta wamelewa
  Kaona nyumba za wageni
  Wenyeji wanagawana ukimwi
 2. Kwa zahanati kuna foleni
  Vijana wanavinyonga vichanga
  Usiku kucha, dodo mapanga
  Vijana watafuta utajiri
 3. Wengine hao barabarani
  Wanauza hekalu la Roho Mungu
  Kisigizio, ajira haba
  Wateja wao ni wazazi wao
 4. Na majasira wanageuza
  Miili yao kufanya mabomu
  Wakidanganywa ati dhawabu
  Kumbe adhabu wanajitwalia
 5. Tubuni sana salini ninyi
  Jahazi lenu limeshatoboka
  Ombeni yeye awahifadhi
  Kwenye tundu la ubavuni mwake