Yu Mwangu kweli Mungu
Yu Mwangu kweli Mungu |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Composer | (traditional) |
Views | 1,541 |
Yu Mwangu kweli Mungu Lyrics
- Yu mwangu kweli Mungu a, yu nami si uongo,
Naye mamoja nangu a, niliye mdude mdogo,
Ee Rabbi nakuungama, ndiwe mkombozi wangu
Mwenyezi, mwenezi, mtoaji wa neema
Mwenyezi, mwenezi, mtoaji wa neema
- Na haya kwani mdhambi mno, nawe mtukufu
Ee mambo yasiyo mfano, mpenda utakatifu
Nakuabudu mi mjao, tayari masikanio
Kwenenda, kutenda, kwa kila amriyo
Kwenenda, kutenda, kwa kila amriyo
- Walakini mi mdhaifu, kusema sikufanya
Hivyo nilivyo mkosefu, hata naona haya
Ee Rabbi wezesha moyo, wangu hutia neemayo
Utake, ushike, yote mapenziyo
Utake, ushike, yote mapenziyo