Chakula cha Watoto

Chakula cha Watoto
Performed by-
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerMartin M. Munywoki
Views3,154

Chakula cha Watoto Lyrics

  1. Si sawa kuchukua chakula cha watoto (si sawa)
    Na kuwatupia mbwa chakula cha watoto (lakini)
    Hata mbwa hula makombo yaangukayo
    (kutoka) mezani mwa Bwana wao
    Nami natamani kuonja chakula hiki
    (ulicho) waandalia wanao
    Japo sifai mimi nakusihi Bwana, uniruhusu tu *2

  2. Nakutamani sana, Bwana wangu (mwema),
    Kujongea karamuni,
    Ijapokuwa mimi sina moyo safi,
    Nina njaa nina kiu niruhusu tu
  3. Nimejawa na dhambi, na uchafu (mwingi),
    Na nimeoza moyoni
    Mawazo mabaya na matendo maovu,
    Hata naona aibu, niruhusu tu
  4. Nisipokupokea, mwili wako (Bwana),
    Sina uzima milele
    Sasa niende wapi zaidi ya kwako,
    Nisamehe nipokee niruhusu tu
  5. Maana ulikuja, duniani (kwao),
    Wenye dhambi kama mimi
    Ulikula nao hata ukafa nao,
    Na mimi nakuhitaji niruhusu tu