Chakula cha Watoto

Chakula cha Watoto
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerMartin M. Munywoki
SourceNairobi Kenya
ReferenceMt. 15.26
Musical Notes
Time Signature3
4
Music KeyG Major
NotesOpen PDF

Chakula cha Watoto Lyrics

Si sawa kuchukua chakula cha watoto (si sawa)
Na kuwatupia mbwa chakula cha watoto (lakini)
Hata mbwa hula makombo yaangukayo
(kutoka) mezani mwa Bwana wao
Nami natamani kuonja chakula hiki
(ulicho) waandalia wanao
Japo sifai mimi nakusihi Bwana, uniruhusu tu *2

 1. Nakutamani sana, Bwana wangu (mwema),
  Kujongea karamuni,
  Ijapokuwa mimi sina moyo safi,
  Nina njaa nina kiu niruhusu tu
 2. Nimejawa na dhambi, na uchafu (mwingi),
  Na nimeoza moyoni
  Mawazo mabaya na matendo maovu,
  Hata naona aibu, niruhusu tu
 3. Nisipokupokea, mwili wako (Bwana),
  Sina uzima milele
  Sasa niende wapi zaidi ya kwako,
  Nisamehe nipokee niruhusu tu
 4. Maana ulikuja, duniani (kwao),
  Wenye dhambi kama mimi
  Ulikula nao hata ukafa nao,
  Na mimi nakuhitaji niruhusu tu