Alidharauliwa na Kukataliwa
Alidharauliwa na Kukataliwa | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | Martin M. Munywoki |
Views | 4,721 |
Alidharauliwa na Kukataliwa Lyrics
Alidharauliwa na kukataliwa kukataliwa na watu
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko- Alikua mbele zake kama mche mwororo,
Na kama mzizi katika nchi nchi kavu
Hakuwa na umbo kuvutia wala uzuri,
Hata tumwonapo tumtamani
Ni kama mtu ambaye watu humficha uso,
Wala hatukumhesabia kuwa kitu - Hakika amechukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu amejitwika.
Lakini na sisi tulidhani kuwa kapigwa,
Amepigwa na Mungu na kuteswa
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu maovu yetu - Adhabu ya amani yetu ilikuwa kwake,
Na kwa kupigwa kwake yeye sisi tumepona
Sisi sote kama ko-ndoo tumepotea,
Kila mmoja njia yake yeye,
Bwana ameweka juu yake maovu yetu,
Alione-wa lakini alinyenyekea - Alionewa lakini hakufunua kinywa,
Kama mwanakondoo akipelekwa machinjoni
Kwa kuonewa kuhukumiwa kaondolewa,
ni nani atasimulia haya?
Ni nani aliyesadiki habari hii?
na mkono wa Bwana amefunuiwa nani?