Alidharauliwa na Kukataliwa

Alidharauliwa na Kukataliwa
Choir-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerMartin M. Munywoki
SourceSt. Paul's Chapel University of Nairobi
ReferenceIsaiah 53
Musical Notes
Timesignature3 4
MusickeyG Major
NotesOpen PDF

Alidharauliwa na Kukataliwa Lyrics


Alidharauliwa na kukataliwa kukataliwa na watu
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko1. Alikua mbele zake kama mche mwororo,
Na kama mzizi katika nchi nchi kavu
Hakuwa na umbo kuvutia wala uzuri,
Hata tumwonapo tumtamani
Ni kama mtu ambaye watu humficha uso,
Wala hatukumhesabia kuwa kitu

2. Hakika amechukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu amejitwika.
Lakini na sisi tulidhani kuwa kapigwa,
Amepigwa na Mungu na kuteswa
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu maovu yetu

3. Adhabu ya amani yetu ilikuwa kwake,
Na kwa kupigwa kwake yeye sisi tumepona
Sisi sote kama ko-ndoo tumepotea,
Kila mmoja njia yake yeye,
Bwana ameweka juu yake maovu yetu,
Alione-wa lakini alinyenyekea


4. Alionewa lakini hakufunua kinywa,
Kama mwanakondoo akipelekwa machinjoni
Kwa kuonewa kuhukumiwa kaondolewa,
ni nani atasimulia haya?
Ni nani aliyesadiki habari hii?
na mkono wa Bwana amefunuiwa nani?

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Zaeni Matunda Mema 5814860
Huniongoza Mwokozi 5814856
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442