Alidharauliwa na Kukataliwa

Alidharauliwa na Kukataliwa
Performed by-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerF. B. Mallya
Views4,105

Alidharauliwa na Kukataliwa Lyrics

  1. {Alidharauliwa na kukataliwa na watu
    Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko } *2

  2. Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao
    Alidharauliwa wala hatukuhesabu kuwa kitu
  3. Hakika ameyachukua masikitiko yetu
    Amejitwika huzuni yetu
  4. Lakini tulimdhania kuwa amepigwa
    Amepigwa na Mungu na kuteswa
    Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu
    Amechubuliwa kwa maovu yetu