Alidharauliwa na Kukataliwa Lyrics

ALIDHARAULIWA NA KUKATALIWA

@ F. B. Mallya

{Alidharauliwa na kukataliwa na watu
Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko } *2

 1. Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao
  Alidharauliwa wala hatukuhesabu kuwa kitu
 2. Hakika ameyachukua masikitiko yetu
  Amejitwika huzuni yetu
 3. Lakini tulimdhania kuwa amepigwa
  Amepigwa na Mungu na kuteswa
  Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu
  Amechubuliwa kwa maovu yetu
Alidharauliwa na Kukataliwa
COMPOSERF. B. Mallya
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
SOURCETanzania
 • Comments