Misa ya Mtakatifu Veronika
Misa ya Mtakatifu Veronika |
---|
Performed by | - |
Category | Misa (Sung Mass) |
Composer | Martin M. Munywoki |
Views | 5,168 |
Misa ya Mtakatifu Veronika Lyrics
EE BWANA UTUHURUMIE
- Ee Bwana (Bwana Mungu) utuhurumie (ee Bwana)
ee Bwana Mungu (tuhurumie) utuhurumie (ee Bwana ee Mungu Mungu utuhurumie
- Ee Yesu (Kristu) utuhurumie
Ee Yesu Kristu utuhurumie
UTUKUFU
Utukufu (juu) kwa Mungu Mbinguni
Na amani iwe kote duniani (tunakuabudu)
Tunakusifu Bwana twakuheshimu Bwana tunakuabudu
Twakutukuza Bwana twakuheshimu Bwana
- Ewe Bwana Mungu Baba mfalme wa Mbinguni
Tunakushukuru kwa utukufu mkuu, Mungu Baba Mwenyezi
- Ewe Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee
Mwana kondoo Mungu uondoaye dhambi, utuhurumi-e
- Uondoaye dhambi zetu utusikie,
Ewe uketiye kuume kwa Mungu Baba, utuhurumi-e
- U pekee Bwana Mtakatifu na u Kristu
Pamoja naye Roho katika utukufu, wake Mungu milele
ALELUYA
- Aleluya (aleluya) aleluya (aleluya) aleluya aleluya
NASADIKI
Nasadiki (kwa Mungu Baba),
nasadiki (kwa Mungu Mwana)
Nasadiki (kwa Mungu Roho) nasadiki
- Nasadiki kwa Mungu mmoja Baba ye-tu Mwenye-zi
Nasadiki Yesu Kristu mwana wake wa pekee
Nasadiki alipata mwili kwa Roho Mtakati-fu
Nasadiki kazaliwa na Bikira Maria
- Aliteswa alisulubiwa kwa amri ya Pnsyo Pilato
Akafa na akazikwa na kushuka kwa wafu
Alifufuka siku ya tatu na kupaa juu Mbingu-ni
Toka huko tarudi kuhukumu ulimwengu
- Nasadiki kwa Roho Mtakatifu na Kanisa Katoliki
Nasadiki Ushirika wao Watakatifu
Nasadiki ufufuko wa miili na ondoleo la dhambi
Nasadiki uzima wa milele na milele
MTAKATIFU
- Mtakatifu (Bwana Mungu) Mtakatifu (wa Majeshi) *2
Mbingu na dunia zimejaa zimejaa
Zimejaa utukufu wako Bwana
- {Hosanna juu Mbinguni Hosanna Mbinguni juu Hosanna juu } *2
Amebarikiwa amebarikiwa yeye
Yeye ajaye kwa jina lake Bwana
FUMBO LA IMANI
- Yesu Kristu alikufa Yesu alifufuka
Atarudi Yesu atakuja tena
AMINA
- Amina (amina) amina (amina) amina amina
BABA YETU
- Baba Yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe daima
Na ufalme wako na ufike na mapenzi yako yatimilike
Utakalo (utakalo) lifanyike (lifanyike) duniani (duniani) kama Mbinguni *2
- Tupe leo na mkate wetu tupe mkate wetu wa kila siku
Tusamehe na makosa yetu vile tusameheavyo wengine
- Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni
Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni
- Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu
Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu
MWANA KONDOO WA MUNGU
- Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie
- Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie
- Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
Tupe amani (tupe amani) utupe amani