Misa ya Mtakatifu Veronika Lyrics

MISA YA MTAKATIFU VERONIKA

@ Martin M. Munywoki

EE BWANA UTUHURUMIE

 1. Ee Bwana (Bwana Mungu) utuhurumie (ee Bwana)
  ee Bwana Mungu (tuhurumie) utuhurumie (ee Bwana ee Mungu Mungu utuhurumie
 2. Ee Yesu (Kristu) utuhurumie
  Ee Yesu Kristu utuhurumie

UTUKUFU

Utukufu (juu) kwa Mungu Mbinguni
Na amani iwe kote duniani (tunakuabudu)

Tunakusifu Bwana twakuheshimu Bwana tunakuabudu
Twakutukuza Bwana twakuheshimu Bwana

 1. Ewe Bwana Mungu Baba mfalme wa Mbinguni
  Tunakushukuru kwa utukufu mkuu, Mungu Baba Mwenyezi
 2. Ewe Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee
  Mwana kondoo Mungu uondoaye dhambi, utuhurumi-e
 3. Uondoaye dhambi zetu utusikie,
  Ewe uketiye kuume kwa Mungu Baba, utuhurumi-e
 4. U pekee Bwana Mtakatifu na u Kristu
  Pamoja naye Roho katika utukufu, wake Mungu milele

  ALELUYA

  • Aleluya (aleluya) aleluya (aleluya) aleluya aleluya

  NASADIKI

  Nasadiki (kwa Mungu Baba),
  nasadiki (kwa Mungu Mwana)
  Nasadiki (kwa Mungu Roho) nasadiki

   1. Nasadiki kwa Mungu mmoja Baba ye-tu Mwenye-zi
    Nasadiki Yesu Kristu mwana wake wa pekee
    Nasadiki alipata mwili kwa Roho Mtakati-fu
    Nasadiki kazaliwa na Bikira Maria
   2. Aliteswa alisulubiwa kwa amri ya Pnsyo Pilato
    Akafa na akazikwa na kushuka kwa wafu
    Alifufuka siku ya tatu na kupaa juu Mbingu-ni
    Toka huko tarudi kuhukumu ulimwengu
   3. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu na Kanisa Katoliki
    Nasadiki Ushirika wao Watakatifu
    Nasadiki ufufuko wa miili na ondoleo la dhambi
    Nasadiki uzima wa milele na milele

    MTAKATIFU

    • Mtakatifu (Bwana Mungu) Mtakatifu (wa Majeshi) *2
     Mbingu na dunia zimejaa zimejaa
     Zimejaa utukufu wako Bwana
    • {Hosanna juu Mbinguni Hosanna Mbinguni juu Hosanna juu } *2
     Amebarikiwa amebarikiwa yeye
     Yeye ajaye kwa jina lake Bwana

    FUMBO LA IMANI

    • Yesu Kristu alikufa Yesu alifufuka
     Atarudi Yesu atakuja tena

    AMINA

    • Amina (amina) amina (amina) amina amina

    BABA YETU

    1. Baba Yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe daima
     Na ufalme wako na ufike na mapenzi yako yatimilike

     Utakalo (utakalo) lifanyike (lifanyike) duniani (duniani) kama Mbinguni *2

    2. Tupe leo na mkate wetu tupe mkate wetu wa kila siku
     Tusamehe na makosa yetu vile tusameheavyo wengine
    3. Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni
     Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni
    4. Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu
     Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu

     MWANA KONDOO WA MUNGU

    1. Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
     Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
     Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie
    2. Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
     Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
     Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie
    3. Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
     Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
     Tupe amani (tupe amani) utupe amani
    Misa ya Mtakatifu Veronika
    COMPOSERMartin M. Munywoki
    CATEGORYMisa (Sung Mass)
    MUSIC KEYKey G
    • Comments