Watikisa Kibuyu
Watikisa Kibuyu |
---|
Performed by | Same KMJ |
Album | Watikisa Kibuyu |
Category | Tafakari |
Composer | E. A. Minja |
Views | 10,380 |
Watikisa Kibuyu Lyrics
Nini siri ya moyo wako kupenda kuwa mtu wa roho mbaya?
Daima moyo wako wasononeka kwa kujiuliza kwa nini?
Jirani yako anapofanikiwa moyo wako wakosa raha
Si zuri si jema moyo wako wakutesa ukiwaza kwa nini!
Na tazama sasa- unachokifanya,
Ni kukimbilia - kutikisa kibuyu
Na imani yako - ni kwenye kibuyu na kibuyu ndiye mungu wako
- Wengine wanakiita ni kinga na kukifanya kama mungu wao
Na tena jina jingine ni 'kimo' sababu yake na kiza ni wivu
Unajisifia ni mtu mwema mwenye roho iliyo na huruma
Lakini kwa ndani wewe mbaya roho imetawaliwa na wivu!
Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu!
Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu!
- Mtoto wa jirani kafaulu katika kazi au ni masomo
Ukijua wakiwaza kibuyu ugeuze miguu yake nyuma
Wenzako wanaongeza bidii ya kujituma kwenye kazi zao
Wewe unawatazama vibaya na kuanza kukiwaza kibuyu
Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu
Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu
- Unapomtazama ndugu yako kajenga nyumba na inapendeza
Ukiitazama moyo wauma sasa wawaza huyu asiishi!
Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu!
Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu!
- Sasa jifikirie ndugu wewe badili roho yako yenye wivu
Na kuutengeneza moyo wako ukafanane nao malaika
Ukirudi kazi kwako ni moja ni kupiga magoti na kusali
Ah! Kumbe waomba upendo uwepo duniani