Sauti za Kuimba
Sauti za Kuimba |
---|
Performed by | - |
Category | Utume wa Uimbaji |
Composer | Martin M. Munywoki |
Views | 26,429 |
Sauti za Kuimba Lyrics
Sauti za kuimba ni talanta zawadi (Tumepewa ) na Mungu tumwimbie } *2
Haya basi nyanyukeni tumsifu
{Ninyi waimbaji (pazeni) zipaazeni sauti (hubirini) kwa sauti zenu } *2
- Mwimbieni Bwana kwa ala za muziki zote zenye sauti tamu
Mpigieni ngoma na baragumu
Aee za muziki zote zenye sauti tamu
Mpigieni ngoma na baragumu
- Jongeeni enyi watunzi wachezaji wa vinanda na waimbaji
Jiungeni nasi sifiche vipaji
Aee wachezaji wa vinanda na waimbaji
Jiungeni nasi sifiche vipaji
- Sauti ya kwanza na pili wapendeza wanapoimba pamoja na
Na sauti ya tatu na nne ona
Aee wapendeza wanapoimba pamoja na
Na sauti ya tatu na nne ona
- Kusifu kwapendeza sana duniani pia mbinguni ni furaha
Haya msifuni kuimba ni raha
Aee duniani pia mbinguni ni furaha
Haya msifuni kuimba ni raha
- Kuimba huondoa dhiki ni faraja kwa waliokata tamaa
Ama burudani kwa walozubaa
Aee ni faraja kwa waliokata tamaa
Ama burudani kwa walozubaa
- Sauti zenu ni talanta amueni jinsi mtazi-tumia
Angalieni mimi ninamwimbia
Aee amueni jinsi mtazi-tumia
Angalieni mimi ninamwimbia