Maneno Saba ya Yesu Msalabani
| Maneno Saba ya Yesu Msalabani | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Album | Mtazame Mkombozi Msalabani |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | E. Z. Ng |
| Views | 17,860 |
Maneno Saba ya Yesu Msalabani Lyrics
- Baada ya kuteswa na kusulubiwshwa msalabani
Aliona walichokifanya hawakukijua
Aliwaombea kwa Mungu akisema
Baba uwasamehe hawalijui wanalofanya - Kulikuwa mhalifu liyemtambua kuwa yeye ni Mungu
Alitubu akaambiwa
Nakuambia hakika leo, utakuwa pamoja nami peponi - Alitukabidhi kwa mama yake
Na huyo ndiyo mwombezi wetu aliposema
Mama tazama huyu ndiye mwanao
Tazama huyu ndiye mamako - Aliona kiu baada ya mateso makali
Hadi alisema mwenyewe naona kiu - Baada ya mateso makali hayo
Aliyoteswa kwa ajili ya dhambi zetu
Aliona yote aliyotumwa na Mungu kuwa yametimia
Aliposema Yametimia *2 - Ndipo alipolia kwa uchungu na kumbwambia Baba
Eloi eloi lamasabakidani, Mungu wangu Mbona umeniacha - Mwisho kabisa aliikabidhi roho yake kwa Baba
Akisema Baba mikononi mwako Naiweka Roho yangu