Maneno Saba ya Yesu Msalabani

Maneno Saba ya Yesu Msalabani
ChoirTBA
AlbumMtazame Mkombozi Msalabani
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerE. Z. Ng
SourceTanzania

Maneno Saba ya Yesu Msalabani Lyrics

 1. Baada ya kuteswa na kusulubiwshwa msalabani
  Aliona walichokifanya hawakukijua
  Aliwaombea kwa Mungu akisema
  Baba uwasamehe hawalijui wanalofanya
 2. Kulikuwa mhalifu liyemtambua kuwa yeye ni Mungu
  Alitubu akaambiwa
  Nakuambia hakika leo, utakuwa pamoja nami peponi
 3. Alitukabidhi kwa mama yake
  Na huyo ndiyo mwombezi wetu aliposema
  Mama tazama huyu ndiye mwanao
  Tazama huyu ndiye mamako
 4. Aliona kiu baada ya mateso makali
  Hadi alisema mwenyewe naona kiu
 5. Baada ya mateso makali hayo
  Aliyoteswa kwa ajili ya dhambi zetu
  Aliona yote aliyotumwa na Mungu kuwa yametimia
  Aliposema Yametimia *2
 6. Ndipo alipolia kwa uchungu na kumbwambia Baba
  Eloi eloi lamasabakidani, Mungu wangu Mbona umeniacha
 7. Mwisho kabisa aliikabidhi roho yake kwa Baba
  Akisema Baba mikononi mwako Naiweka Roho yangu