Simba wa Yuda
Simba wa Yuda | |
---|---|
Alt Title | Tumshangilie Mwokozi Amefufuka |
Performed by | St. Charles Lwanga Yombo Dovya Dsm |
Album | Kafufuka Mwokozi |
Category | Pasaka (Easter) |
Composer | A. J. Msangule |
Views | 10,219 |
Simba wa Yuda Lyrics
Tumshangilie Mwokozi amefufuka
Tupige makofi, pia na vigelegele
Amefufuka Kristu mshindi na ukombozi umekamilika
Kwa ufufuko wake Kristu sisi tumekombolewa
Amefufuka mfalme mshindi, Simba wa Yuda anaonguruma
Na ikulu ya Ibilisi sasa imebomolewa- Amefufuka Mkombozi wetu Yesu Kristu
Kashinda dhambi na mauti ametukomboa
Utawala wa ibilisi umetoweka
Minyororo ya utumwa wa dhambi imeshavunjwa - Mayahudi waliomuua Bwana Yesu
Wameumbuka kwani mkombozi yuko hai
Na lile jiwe walilokataa waashi
Ndilo limekuwa jiwe kuu tena la pembeni - Nasi tukitaka kufufuka naye Kristu
Tuache dhambi za vilema vyetu kudumu
Kwani Yesu aliyefufuka ameleta
Uzima mpya kwa wale watakaobadilika