Simba wa Yuda

Simba wa Yuda
ChoirSt. Charles Lwanga Yombo Dovya Dsm
AlbumKafufuka Mwokozi
CategoryPasaka (Easter)
ComposerA. J. Msangule
SourceDar-es-Salaam Tanzania

Simba wa Yuda Lyrics


Tumshangilie Mwokozi amefufuka
Tupige makofi, pia na vigelegele
Amefufuka Kristu mshindi na ukombozi umekamilika
Kwa ufufuko wake Kristu sisi tumekombolewa
Amefufuka mfalme mshindi, Simba wa Yuda anaonguruma
Na ikulu ya Ibilisi sasa imebomolewa


1. Amefufuka Mkombozi wetu Yesu Kristu
Kashinda dhambi na mauti ametukomboa
Utawala wa ibilisi umetoweka
Minyororo ya utumwa wa dhambi imeshavunjwa

2. Mayahudi waliomuua Bwana Yesu
Wameumbuka kwani mkombozi yuko hai
Na lile jiwe walilokataa waashi
Ndilo limekuwa jiwe kuu tena la pembeni

3. Nasi tukitaka kufufuka naye Kristu
Tuache dhambi za vilema vyetu kudumu
Kwani Yesu aliyefufuka ameleta
Uzima mpya kwa wale watakaobadilika

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Zaeni Matunda Mema 5814860
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Huniongoza Mwokozi 5814856
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442