Ameenea

Ameenea
ChoirSt. Augustine University of Dsm
AlbumNamtegemea Mungu
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerBernard Mukasa
Musical Notes
Time Signature6
16
Music KeyD Major
NotesOpen PDF

Ameenea Lyrics

// utangulizi //

Sijaona (tena) sijaona (miye) aliye mwema kama hivi
Amejaa (tele) amejaa (huyu) huruma neema na faraja
Hanyamazi (kamwe) hanyamazi (yeye) tunapomwita huitika
(Naye) amekuwa (kwetu) ni mwaminifu tena mkweli mpaji

// kiitikio //

Na kila kitu tunachomuomba Mungu, Yeye anatujibu
Na kila jambo tunalomuomba Bwana, Yeye anatujibu
Na kila mara tukisemezana naye, Yeye anatujibu
Na kila jambo tunalomuomba sisi, Yeye anatujibu
Na tena hashindwi jambo na hamtupi mtu
Yeye hashindwi jambo na hamtupi mtu

// mashairi //

 1. Yote mahitaji yetu, tunaomba anatupa
  Hata tusiyoyajua, nayo anateremsha
  Wa ajabu, ha ha nashindwa nieleze vipi
 2. Mambo yakiwa magumu, ujasiri anatupa
  Tunayabeba vilivyo, te na kwa uvumilivu,
  Wa ajabu, ha ha kwa kweli ananishangaza
 3. Siku ya kija manono, atupa uadilifu
  Tupokee kwa uchaji, yeye awe mtukufu
  Wa ajabu, ha ha ajabu ni ajabu tupu

  // hitimisho //

  Heri na neema ndiye anatoa
  Nguvu na uzima anatujalia
  Nayo mafanikio he anatoa yeye
  Kupata watoto (wazuri) ni neema zake (siyo ujanja)
  Kupata elimu (ya juu) ni baraka zake (siyo akili)

  Yupo kila mahali Mungu ameenea
  Pote anasikia sana akiitwa anaitika
  Yupo kila mahali Mungu ameenea
  Pote kweenye mitego mikuu hata mapito ya kutisha
  Yupo kila mahali Mungu ameenea
  Yote tunayoyajua na tusiyoyatambua
  Yupo kila mahali Mungu ameenea

  Yupo kila mahali tu, yupo kila mahali tu
  Yupo kila mahali Mungu ameenea
  Ameenea ameenea, ameenea, ameenea
  Ameenea ameenea, ameenea, ameenea
  Kila mahali ni yeye Mungu ameenea