Njia za Mkato
Njia za Mkato |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | Martin M. Munywoki |
Views | 3,028 |
Njia za Mkato Lyrics
- // utangulizi //
Haraka hara-ka haina baraka,
(ndugu yangu) ka-wia ufike uendapo salama
Jifunze subi-ra na uvumilivu,
(fanya kazi) usipende kupata vya rahisi vya bure
Haupendi kuchoka - wala kutoa jasho
Wategemea - mali ya ndugu yako
Haupendi kungoja - wala kuulizia
Unafuata - njia za vichochoro!
// kiitikio //
Njia za mkato ee -
Njia za mkato ee ni hatari sana
Zenye mabonde na maporomoko ee-
Na maporomoko ee ni hatari sana
Hizo za vichochoro ee-
Za vichochoroni ee ni hatari sana
Humo wamejaa na wanyang'anyi ee-
Nao wanyang'anyi ee ni hatari sana jihadhari sana
// mashairi //
- Mbona unataka mali upesi pasipo kutoa jasho
Vijia vya mkato unavipenda
Unaiba wala rushwa unavuna usikopanda
Majibu ya haraka unayapenda
- Mbona unafurahia uzinzi pasipo kufunga ndoa
Vijia vya mkato unavipenda
Unapolemewa na ndoa wamkimbilia mganga
Majibu ya haraka unayapenda
- Mbona unapokosea wewe wajitetea kwa uongo
Vijia vya mkato unavipenda
Unapokosana na ndugu wasuluhisha kwa vita
Majibu ya haraka unayapenda