Tuvumiliane
| Tuvumiliane |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Tafakari |
| Composer | Martin M. Munywoki |
| Views | 3,115 |
Tuvumiliane Lyrics
Tuvumiliane tuvumiliane, tuishi kwa upendo nao wenzetu
Tuwakubali hao jinsi walivyo, ijapokuwa hawafanani nasi
- Wapo walio masikini wahitaji, miongoni mwetu
Tusiwachoke wanapoombaomba, tuwavumilie
Wengine hawana elimu kama sisi, miongoni mwetu
Tuwaeleze kwa upole na pia, tuwavumilie hivyo
- Wengine wa asili tofauti nasi, miongoni mwetu
Tusizidharau tamaduni zao, tuwavumilie
Pia wapo wengi wa dini mbali mbali, miongoni mwetu
Tusiwahukumu kwa imani yao, tuwavumilie hivyo
- Malezi na mapito yetu sio sawa, miongoni mwetu
Wengine wameona machungu mengi, tuwavumilie
Wengine hukasirika haraka sana, miongoni mwetu
Tusiwe sababu ya machozi yao, tuwavumilie hivyo