Uhuru wa Kweli

Uhuru wa Kweli
Performed bySt. Maria Goretti Mbagala
AlbumUhuru wa Kweli
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views2,854

Uhuru wa Kweli Lyrics

  1. //utangulizi

    Ninyi mliitwa ndugu muwe watu huru kabisa
    Lakini uhuru huo sio wa kuusingizia
    Isiwe ni sababu - ya kutawaliwa na tamaa hizi
    Tamaa za dunia - msitawaliwe na tamaa za dunia
    Ooh jifunzeni kutumikiana kwa upendo daima
    Kwani sheria ni moja nayo ndiyo upendo

    //kiitikio

    Uhuru wangu ee - uhuru wangu
    Uhuru wangu wa thamani
    Uhuru wangu jamani - uhuru wangu (uhuru)
    Unatokana na ukweli

  2. Nikijisifu kwa uongo, nateseka
    Kwani siwezi dhihirisha sifa yenyewe
    Jamii itatarajia kutoka kwangu
    Nisiyoweza kuyatenda, kwani si ya kweli!
  3. Nikifanya udanganyifu, kwenye fedha
    Nikimwona ausikaye ninazizima
    Au nikipokea rushwa, nitanena
    Hata yale yasiyo mema, yanidhalilishe!
  4. Nikikosa uaminifu, kwenye ndoa
    Nitakwepa kuongozana, na mpendwa wangu
    Ili tusije kukutana, na hawara
    Akashindwa kuvumilia, akanipondeza!
  5. Nikizunguka nchi nzima, kuongea
    Uwogo juu ya mwenzangu, najiumiza
    Tukikutana ana njaa, yuko kimya
    Nitadhani wamemwambia, nitapata hofu
  6. Nikimtesa mpwa wangu, nimleaye
    Sitatamani aonane na wazazi wake
    Kwani najua atasema, nimtendeayo
    Na mimi nitadhalilika, nitaaibika!
  7. Nikifanya upendeleo, ofisini
    Kumkweza asiyefaa, najidhihaki
    Jamii ikimhubiri, afaaye
    Nitahisi nakejeliwa na kuunguliwa

    // hitimisho
    ---
    Kwa sababu mimi, ndiye, ninaiandika mwenyewe
    Historia yangu, leo, itakayosomwa milele
    Daima milele, daima milele, daima milele
    Muamuzi wangu ndimi!