Nashukuru Bwana
   
    
     
         
          
            Nashukuru Bwana Lyrics
 
             
            
- Nashukuru Bwana, ee Bwana nashukuru sana
 Kwa yote yote, uliyonijalia mimi kiumbe chako,
 Niliye mdogo mbele yako
 Nitaimba sifa zako ooo milele na milele
- Siku zote, Bwana wanipa mkate
 Japo kidogo, silali njaa, hata siku moja
- Shamba langu, nimepanda nimepata,
 Mazao mengi, yapo ghalani, ghalani mwangu
- Unanipa, nguvu za kuwashinda
 Wanaoniwinda, mwili na roho, wanimalize
- Bila wewe, mimi siwezi kitu,
 Vitu vyote, nilivyo navyo, nimepata kwako
- Wema wako, kwangu mimi mwanao,
 Haupimiki, nashukuru Bwana, nashukuru Bwana