Login | Register

Sauti za Kuimba

Nashukuru Bwana Lyrics

NASHUKURU BWANA

@ Stanslaus Mujwahuki

Nashukuru Bwana, ee Bwana nashukuru sana
Kwa yote yote, uliyonijalia mimi kiumbe chako,
Niliye mdogo mbele yako
Nitaimba sifa zako ooo milele na milele

 1. Siku zote, Bwana wanipa mkate
  Japo kidogo, silali njaa, hata siku moja
 2. Shamba langu, nimepanda nimepata,
  Mazao mengi, yapo ghalani, ghalani mwangu
 3. Unanipa, nguvu za kuwashinda
  Wanaoniwinda, mwili na roho, wanimalize
 4. Bila wewe, mimi siwezi kitu,
  Vitu vyote, nilivyo navyo, nimepata kwako
 5. Wema wako, kwangu mimi mwanao,
  Haupimiki, nashukuru Bwana, nashukuru Bwana
Nashukuru Bwana
COMPOSERStanslaus Mujwahuki
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYB Flat Major
TIME SIGNATURE6
16
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments