Nampenda Bwana Mungu
| Nampenda Bwana Mungu |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Zaburi |
| Composer | Fr. Aloyce Msigwa |
| Views | 4,683 |
Nampenda Bwana Mungu Lyrics
Nampenda Mungu muumba wangu
kwa maana amenisikiliza;
Amekisikia kilio changu maombi
yangu ameyapokea; nilipokuwa
taabuni (yeye) alinishika mkono
( tena) kifo kiliponisonga ( Mungu)
aliniponya salama
- Hatari ya kifo ilinizunguka na
vitisho vya kaburi, vilinivamia
nikajawa na mahangaiko ya majonzi.
- Nikamlilia Mwenyezi Mungu kwa
kelele zenye hofu, kwa huruma yake
akaniponya ee Mungu tegemeo langu
- Mungu huwalinda wanyofu wa
moyo wasipatwe na mikasa,
wakikandamizwa huwaokoa maana
yeye mwaminifu