Nimemkataa Shetani

Nimemkataa Shetani
Performed bySt. Monica Lower Kabete Campus UoN
CategoryTafakari
ComposerEvans Kibet
Views3,490

Nimemkataa Shetani Lyrics

  1. Je je, umemkataa shetani huyo na mambo yake yote
    Nimemkataa shetani na vishawishi vyake vyote
    Je je, umemkataa shetani huyo na ila zake tamu
    Nimemkataa shetani na mazingaombwe yake
    Mtazame huyo mwovu na chengachenga zake,
    Huja pole pole,mwenye stara zake,
    malaika wa mwangaza yuaja kunizuzua
    Bwana ninakuomba macho nifungue,
    nipate kuyajua, mema na mazuri,
    ya ufalme wako, niyaache ya shetani

  2. Mungu kaniinua, kanitoa kwenye shimo,
    alimokua yule mwovu kanitia pingu,
    sasa niko huru, ninatabasabu,
    nitamuinua nitasema mimi nimemkataa shetani
  3. Sina hofu mimi,sina haya kumsifu,
    aliyeshinda vita hivyo sasa mimi mzima,
    nami nitafuata,njia zake hata,
    mwisho wa dahari ama kweli mimi nimemkataa shetani
  4. Chenga chenga zake,n imeasi tena sana,
    majaribun hayo sina budi kuyahepa mimi,
    nitaishika kweli Imani sitakubali anishinde mimi nimemkataa shetani.