Tuwatunze Watoto
Tuwatunze Watoto |
---|
Performed by | - |
Album | Toba Yangu |
Category | Familia |
Composer | Bontuta Boniface |
Views | 3,616 |
Tuwatunze Watoto Lyrics
Watoto wetu ni Baraka tu,na tuwatunze watoto wetu,
hawataacha njia, Mwenyezi, kwa neema anayowajalia
(basi wapenzi) tulee watoto kwa mapendo,
(hivyo ndugu) tulee watoto kwa hekima nao waimarike
(ni baraka) tulee watoto kwa hekima nao waimarike.
- Ni bahati kabisa tuliyojaliwa,
tujitolee kuwalea ipasavyo ha!
Na kuwafunza yaliyo mema kijamii
- Kweli wengine wanahusisha watoto,
wadogo kwa mambo yasiyoeleweka ha!
Na kuwafunza yasiyofaa kijamii
- Tusiwatese watoto Mungu asema,
acheni wote waje kwangu nawapenda ha!
Tuwafundishe yale yanayostahili
- Na vile watoto uwaleavyo wewe,
usiwanyime haki zao uwalinde we!
Uwapende uwatunze uwatumikie