Unavyozidi Kukawia

Unavyozidi Kukawia
ChoirMtoni Choir
AlbumMtazame Mkombozi Msalabani
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerBernard Mukasa

Unavyozidi Kukawia Lyrics

Unavyozidi kukawia, kunisaidia Bwana,
Ndivyo na mimi, ninavyozidi kukutumainia wewe tu *2

  1. Nimejaa dhambi, hivyo nafahamu,
    Sistahili kuhurumiwa nawe
  2. Ningekuwa mwema, ukelele wangu,
    Ungefika masikioni mwako
  3. Ninavyojitahidi kukulilia,
    Ndivyo ninavyozidi kuteseka