Maneno

Maneno
Performed byBMT Ledochowska K/Ndege Dodoma
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerBernard Mukasa
Views5,696

Maneno Lyrics

  1. Tazama nimesikia nimesikia mahusia yako,
    Tazama nimeelewa nimeelewa maagizo yako
    Ee Bwana nimevutiwa, nimevutiwa nayo njia yako
    Ee Bwana nimeamua kuyapokea mafundisho yako
    Tazama nimesikia tazama mahusia tazama nimesikia na nimeelewa
    Na ninainuka sasa ninakuja

    { Natembea kwa imani ninakuja hapo ulipo
    Tena kwa matumaini ninakuja hapo ulipo
    Uyaweke maneno maneno yako kinyani mwangu
    Nikahubiri maneno yako kwa ulimwengu } *2

  2. Nakumbuka ulivyoahidi kuwa nami kila mahali
    Na kunifundisha lugha nitakayoizungumza
    Tena utakavyonipa nguvu barazani mwa watawala
    Watakapotaka kunihukumu kusudi waufiche ukweli
  3. Tena umenitahadharisha nitapigwa na maadui
    Kama kondoo kati ya mbwa mwitu nitavamiwa
    Naomba neema yako Bwana ili nisikate tamaa
    Ujumbe wangu niufikishe kwa watu bila kuvunjika moyo
  4. Haya yote yakakupe wewe utukufu sifa heshima
    Utukuzwe Mungu Baba Mwana na Roho Mtakatifu
    Kama vile vile ilivyokuwa mwanzo na ilivyo sasa
    Utukuzwe vivyo hivyo Mungu daima hata milele milele

    < hitimisho >
    Maneno maneno yako kinywani mwangu
    Hubiri maneno yako kwa ulimwengu
    Uyaweke maneno yako kinywani mwangu
    Niende nikahubiri maneno yako kwa watu wote