Kaeni Katika Pendo
| Kaeni Katika Pendo |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Love |
| Composer | Stanslaus Mujwahuki |
| Views | 5,901 |
Kaeni Katika Pendo Lyrics
Kama vile Baba alivyonipenda mimi
Nami nilivyo wapenda ninyi
Kaeni katika pendo langu
Kaeni - katika pendo (langu) * 2
Kaeni katika pendo langu
- Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu
Kama vile mimi nilivyozishika, amri za Baba yangu
Na kukaa katika pendo lake
- Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu
Na furaha yenu itimizwe
- Amri yangu ndiyo hii, mpendane kama nilivyowapenda
Kama nilivyowapenda ninyi
- Hamna aliye na upendo, upendo mwingi kuliko huu
Wa mtu kutoa uhai wake, kwa ajili ya rafiki zake