Ahadi

Ahadi
ChoirBMT Ledochowska K/Ndege Dodoma
AlbumSinodi Afrika
CategoryTafakari
ComposerChristian Charles

Ahadi Lyrics

 1. Niliyafumbua macho yangu nikatazama,
  Ili nimuone ashukapo toka winguni
  Maana aliniahidi kuwa atarudi
  Kunichukua tukafurahi pamoja naye Mbinguni

  Ilikuwa hamu ya moyo wangu tazama
  Na bado ninatamani kipi kitanizuia
  Niuone uso wa Bwana na Mungu wangu
  Nimuone akiitimiza ahadi yake

 2. Kaniahidi nikivumilia mpaka mwisho
  Nitamuona katika kiti chake cha enzi
  Akanionya nijitenge mbali na wazushi
  Wasije wakaipotosha imani yangu, hakika
 3. Nijapoanguka katika dhambi ya mauti
  Ataiosha ikawa nyeupe kama suti
  Na tena nikimlilia katika ukunga
  Atanipa uzao kama nyota za mbinguni, ajabu
 4. Kwa hiyo moyo wangu umetulia kabisa
  Kwa kuwa nimejua kwamba ipo tumaini
  Atukuzwe Baba Mwana na Roho Mtakatifu
  Kama ilivyo mwanzo, sasa na milele yote amina