Siri ya Moyo Wangu
   
    
     
         
          
            Siri ya Moyo Wangu Lyrics
 
             
            
- {Siri ya moyo wangu, ni kilio changu
 Na kilio cha moyo wangu, niione huruma yako } *2
 Mungu wangu kinga yangu, nakuita Bwana
 Ukinigeuka wewe nimekwisha mimi
 Wewe ndiwe fimbo yangu, kimbilio langu
 Ndiwe boma la wokovu, msaada wangu
 Niepushie makucha ya dunia
- Kikombe cha uchungu nimekunywa kwa harakwa
 Sasa kimenikwama
 Nimenaswa nimefikwa yamenikuta mimi
 Ee Bwana ninakuita mimi ee Mungu njoo unikamilishe
- Najua haina thamani, sala yangu ni chafu
 Ibada haifai
 Nimkimbilie nani zaidi yako wewe
 Naililia huruma yako, mkono wako nishike Bwana
- Mimi sistahili kabisa kupokea neema
 Kutoka kwako Bwana
 Ni mchafu ni mdhambi, nimeoza moyoni
 Mikono nakuinulia Bwana, machozi yangu nafukia mimi