Ametamalaki
Ametamalaki Lyrics
- Njooni na vinanda, ngoma zeze vinubi
Tumpigie Mungu wetu muziki mtakatifu
Ametamalaki - ametamaliki Bwana ametamalaki
Mbinguni ni yeye -
Duniani ni yeye -
Ametamaliki -
- Malaika Mbinguni wanamsifu Mungu
Na duniani pia asifiwaye ni Mungu wa milele
- Asubuhi mapema ndege walialia
Wakisifu pia wakishukuru kwa sauti za shangwe
- Tazama sura yako na ya jirani yako
Muonekano huo ni mfano wake Mwenyezi Mungu
- Uhai wetu uko mikononi mwa Bwana
Autoaye ndiye auchukuaye milele milele
- Uwepo wake unaonekana wazi
Kwa matendo ya huruma ayatendayo kila siku