Asubuhi Imefika
   
    
     
         
          
            Asubuhi Imefika Lyrics
 
             
            
- Asubuhi imefika sasa, usiku umeisha, kumeshapambazuka
 Na mchana umewadia, usiku umeisha, kumeshapambazuka
 Ikawa ni asubuhi
 Viumbe,
 Viumbe vyote vishangilie pilka za hapa na pale
 Kwa kuwa Mungu aliye hai ametulinda
 Tushangilie tuimbe, kwa furaha tuimbe
 Kwa kuwa Bwana ni mwema tumwimbie kwa maringo
- Nguvu tumejaliwa tumeamka na afya njema
 Mungu ametulinda tumeona siku ya leo
 Hivyo basi tumshukuru Muumba
- Nyota zilikuwepo usiku huu wa manene
 Wote tumefumbwa jua tumelala usigizi
 Hivyo basi tumshukuru Mwenyezi