Zakayo Alimwambia Yesu
Zakayo Alimwambia Yesu |
---|
Alt Title | Siku Moja Zakayo |
Performed by | - |
Category | Mafundisho ya Yesu |
Composer | G. A. Chavallah |
Views | 4,677 |
Zakayo Alimwambia Yesu Lyrics
Siku moja Zakayo alimwambia Yesu
Bwana sikiliza mimi nitawapa
Masikini nusu ya mali yangu yote
Bwana sikiliza mimi nitawapa
Masikini nusu ya mali yangu yote
Kama nimemdhulumu mtu nitamrudishia mara nne
(kiasi hicho) nitamrudishia mara nne
- Yesu akamwambia leo wokovu
Umefika katika nyumba hii
Kwa vile huyu pia ni wa ukoo
Ni wa ukoo wa Abrahamu
- Kwa maana mwana wa mtu
Amekuja kutafuta
Na kuokoa kilichopotea
Na kuokoa kilichopotea