Msinyamaze
Msinyamaze | |
---|---|
Alt Title | Ni Vyema Sana Kumwimbia |
Performed by | BMT Ledochowska K/Ndege Dodoma |
Category | Zaburi |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 3,037 |
Msinyamaze Lyrics
MSINYAMAZE
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri (ni kuzuri)
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, (ni kuzuri sana)
Kumfanyia shangwe nyimbo na zaburi
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, kabisa- Fanyeni kanuni moja wapendwa
Kwenu kumwimbia Mungu wenu daima
Maana aliwapeni sauti na vinywa
Hivyo kumwimbia Mungu wenu ni vyema
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, kabisa - Funueni vinywa vyenu wapendwa
Kwani kumwimbia mungu wenu ni heri
kwa kuwa amepita sifa zote za vinywa
Bali kumwimbia Mungu wenu ni vyema
Ni vyema sana kumwimbia Bwana
Kusifu kwapendeza ni kuzuri, kabisa
//hitimisho//
Kuimba msiache msinyamaze
Hata mtokwe jasho msinyamaze
Vijana na wazee msinyamaze
Watoto himahima msinyamaze iyelee