Wewe Petro Utanikana

Wewe Petro Utanikana
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumHii ni Kwaresma
CategoryTBA
Views5,124

Wewe Petro Utanikana Lyrics

  1. { Wewe Petro, nakwambia, utanikana mara tatu
    Kabla ya jogoo kuwika, wewe Petro utanikana } *2

  2. Simoni Petro akamwambi, Bwana unakwenda wapi
    Yesu akamjibu, niendapo huwezi kunifuata sasa
    Lakini utanifuata baadaye
  3. Petro akamwambia, Bwana,
    Kwa nini mimi siwezi kukufuata sasa
    Mimi nitatoa uhai wangu kwa ajili yako
  4. Yesu akamjibu, je wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu
    Amin amin nakuambia wimbi hatawika
    Hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu