Bwana Yesu Twakumbuka
Bwana Yesu Twakumbuka | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Hii ni Kwaresma |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Views | 4,069 |
Bwana Yesu Twakumbuka Lyrics
BWANA YESU TWAKUMBUKA
- Bwana Yesu twakumbuka
Mateso yako makuu
Ili utuokoe sisi
Bustanini Getsemani
Uchungu ukakupata
Ukikumbuka dhambi zetu
Taji la miiba wavikwa
Na mijeredi wapigwa
Ni mateso gani hayo
Jasho la damu latona
Mwili mzima ni mateso
Yote yo kwa ajili yetu - Kwa Pilato unafika
Bure unashtakiwa
Umekosa nini wewe Yesu
Sisi twasitahili hukumu
Sio wewe Bwana Yesu
Ndiyo sisi siyo wewe
Msalaba ni mzito
Umeshinda nguvu zako
Hata chini waanguka
Askari wakupiga
Tena bila ya huruma
We uliye muumba wao - Njiani unaonana
Na mamayo Maria
Mwilio wajaa madonda
Kwa uchungu Mama MAria
Alipomwona mwanaye
Machozi yalimtoka
Huku na huku wakuvuta
Wauwaji hawa wabaya
Kwa nguvu wakutupa chini
Ee Yesu tusaidie
Tujue kutubu hima
Tuangukapo madhambini