Salamu Salamu Malkia wa Mbingu
Salamu Salamu Malkia wa Mbingu Lyrics
Salamu salamu Malkia wa Mbingu
Salamu salamu, Mama wake Mungu
Sisi wana wako, twaja mbele yako
Tupokee mama sisi wana wako
-
Kukupenda wewe ndiyo heri yetu
Kukuomba wewe tumaini letu
Ewe mama mpole, mwenye uso mpole
Utuhurumie utusaidie
-
Yesu kakupenda akakuchagua
Kuwa mama yake akakuteua
Umebarikiwa, umejaa neema
Jina lako Baba litukuzwe pote
-
Hapa duniani utusaidie
Na adui mwovu utuepushie
Utuangalie utusaidie
Ee mama mwezaji utusaidie