Tazama Mama Mwanao
Tazama Mama Mwanao | |
---|---|
Performed by | St. Patrick Morogoro |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Views | 3,993 |
Tazama Mama Mwanao Lyrics
Tazama Mama mwanao, atundikwa msalabani
Sababu gani hi-yo, mwanao kutiwa hatiani
{ Uchungu, mama, uchung,u mama,
Uchungu mama kwa mwanao } *2- [ s ] Sioni kosa lolote, alilolitenda mwanangu
Mwanangu hakuwa na kosa, makosa hayo juu yenu
Uchungu, uchungu, uchungu sana kwa mwanangu *2 - [ t ] Kutundikwa juu msalabani, sababu yake ukombozi
Atukomboe utumwani, tuwe wana wa ukombozi
Ni sisi, ni sisi, ni sisi mama wakosefu *2 - [ s ] Mwanangu haikumpasa, kufa bure bila sababu
Mwanangu Mungu mtu pekee, kwake sioni kosa kwangu
Uchungu, uchungu, uchungu sana kwa mwanangu *2 - [ t ] Kumbuka mama Maria, maneno ya mwanao Yesu
Nitakufa nitafufuka, na kwenda juu kwa Baba yangu
Ya nini, ya nini, ya nini mama huzuni hiyo